Riwaya hii inahusu unyanyasaji wa kijinsia ndoa za utotoni na ukatili katika jamii ya Kiafrika. Inaelezea kwa undani namna changamoto hizi zinavyoathiri maisha ya wasichana na wanawake. Mhusika mkuu ambaye ni msichana mdogo anakabiliana na maisha ya dhuluma ukosefu wa haki na shinikizo la kuolewa akiwa bado mtoto hali inayozuia maendeleo yake ya kielimu na ndoto zake.Katika riwaya hii mhusika mkuu anaonyeshwa akikumbana na unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wanaume wakubwa au hata watu wa karibu katika jamii hali inayomuacha na makovu ya kimwili na kiakili. Pia jamii inaonekana kushindwa kumsapoti huku sheria na haki zikionekana kutotenda haki kwa wanawake na wasichana wanaokandamizwa.Riwaya hii inabainisha changamoto wanazopitia wasichana wanaolazimishwa kuolewa wakiwa watoto mara nyingi kutokana na umaskini au mila potofu zinazoendelezwa kizazi baada ya kizazi. Athari za ndoa hizi zinaonekana katika afya yao elimu na uwezo wa kujikomboa kiuchumi na kiakili.
Piracy-free
Assured Quality
Secure Transactions
Delivery Options
Please enter pincode to check delivery time.
*COD & Shipping Charges may apply on certain items.