Kolonia Santita

About The Book

'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea kwa kinagaubaga jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika Asia Amerika Ulaya - na kung'oa mizizi ya shirika la CS-14 lote katika nchi za Hemisifi a ya Magharibi - na duniani kwa jumla. Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta hali kadhalika ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania Wakenya na Waganda - na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili - na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.
Piracy-free
Piracy-free
Assured Quality
Assured Quality
Secure Transactions
Secure Transactions
Delivery Options
Please enter pincode to check delivery time.
*COD & Shipping Charges may apply on certain items.
Review final details at checkout.
downArrow

Details


LOOKING TO PLACE A BULK ORDER?CLICK HERE