Kolonia Santita

About The Book

Hii ni riwaya ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya inayozu-ngumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa ya kud-hibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC); na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko.

Inaelezea kwa kinagaubaga jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighai ya nyukilia: kwenda Afrika Asia Amerika Ulaya - na kung'oa mizizi ya shirika la CS-14 lote katika nchi za Hemisifia ya Magharibi - na duniani kwa jumla.

Ukisoma kitabu hiki utajiuliza mwandishi huyu aliwezaje kusuka riwaya inayoufanya moyo kukuenda mbio hata kukulazimu wakati mwingine kukiweka kitabu kando ili urudishe pumzi! Ukishakianza tu hutakiacha kabla ya kujua mwisho wa vita hi kali ya kimataifa. Na kivutio kikubwa ni kuwa kiongozi wa vita hiyo kwa upande wa Umoja wa Mataifa ni Murphy Ambilikile Mtanzania - Willy Gamba wa Karne ya 21.

Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta hali kadhalika ufahamu na burudani ya kimataifa kwa wasomaji wa riwaya za kiswahili.

Enock Maregesi ni gwiji wa vandishi wa riwaya za kijasusi na Kolonia Santita imeweka kiwango kipya cha juu kitakachowaumiza vichwa waandishi wengine katika kutaka kukifkia.

Piracy-free
Piracy-free
Assured Quality
Assured Quality
Secure Transactions
Secure Transactions
Delivery Options
Please enter pincode to check delivery time.
*COD & Shipping Charges may apply on certain items.
Review final details at checkout.
downArrow

Details

LOOKING TO PLACE A BULK ORDER?CLICK HERE