HASHIL Seif Hashil alizaliwa kwenye ngarawa katika maji ya bahari ya Pemba Januari 12 1938. Alisoma skuli ya msingi ya Mkwajuni na baadaye katika iliyokuwa Seyyid Khalifa Secondary Technical School Beit-el-Ras Unguja. Alikuwa ni mmoja wa vijana wafuasi wa Abdulrahman Babu waliopelekwa Cuba kwa mafunzo ya kijeshi kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 1964. Baada ya Mapinduzi alipelekwa Indonesia kusomea sayansi ya ubaharia kwa miaka miwili na pia alipelekwa China kusomea uanamaji.Hashil Zanzibar alifanya kazi mbalimbali aliwahi kuwa afisa wa tatu katika meli za MV Africa na MV Jamhuri. Alipouliwa Rais wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume 1972 Hashil alikamatwa na kuwekwa jela ya Ukonga Dar es Salaam kwa muda wa miaka sita. Alipofunguliwa alikwenda Denmark kama mkimbizi. Baada ya miaka mitano akawa raia wa Denmark. Alifanya kazi katika meli mbalimbali za Kideni na baadaye alifanya kazi kwa miaka 20 katika Shirika la Haki za Binadamu la Denmark. Hashil ni mshairi na mwandishi wa vitabu vya riwaya.
Piracy-free
Assured Quality
Secure Transactions
Delivery Options
Please enter pincode to check delivery time.
*COD & Shipping Charges may apply on certain items.