<p>Mstahamilivu hula mbivu mtaka cha uvunguni sharti ainame na mchumia juani hulia kivulini. Ni machache ya maadili yamuongozayo binti Malaika katika safari yake ya kutimiza ndoto zake. Kujiendeleza kielimu ndiyo ndoto yake kuu. Kwa vile Mungu hamtupi mja wake anabahatika kwenda ughaibuni kitaaluma. Ni safari inayomtenganisha na mpenzi wake Ben. Lakini Ben anaahidi kumsubiri hadi afuzu masomo yake. Katika kipindi hiki cha utengano dunia inawapangia mambo mengine kabisa ni utengano unaotishia kulisumu penzi lao. Majaribu hayeshi vishawishi ni vingi. Penzi lao linayumba linatishia kudumbukia kwenye dimbwi la damu. Lakini Malaika haliachii penzi lake kwa Ben analipigania kishujaa. Ben pia anaingia vitani kulipigania penzi la Malaika. Je watashinda vita hivi vya kimapenzi?</p>
Piracy-free
Assured Quality
Secure Transactions
Delivery Options
Please enter pincode to check delivery time.
*COD & Shipping Charges may apply on certain items.