Hiki ni kijitabu cha kusaidia kuokoa Maisha kilicho na njia rahisi ambazo kila mtu anafaa kujua ili kuboresha kinga yake. Watu wengi wamefariki au hata kuugua kwa muda mrefu kwa kukosa ujumbe huu.

Kwa kuanza na njia muhimu zaidi kitabu hiki kitaorodhesha njia zote moja baada ya nyingine ambazo ni rahisi kuzifuata nyumbani . Nyingi ya njia hizi za kuimarisha kinga zilisaidia wanajamii ili kuhakikisha kuwepo kwa asilimia moja pekee ya vifo wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Spanish flu mwaka wa 1918.

Rekodi hii ni ya kipekee haswa ikizingatiwa kuwa nyingi ya hospitali kubwa zilishuhudia asilimia 30-40 ya vifo wakati wa mkasa huo.

Kitabu hiki hakiangazii kupata chanjo kuvaa barakoa kujitenga kutoka kwa wanajamii wengine au kutokaribiana katika shughuli za umma . kinaangazia kuhusu mikakati muhimu ambayo iwapo zitatekelezwa zitachangia pakubwa katika kuimarisha kinga yetu kibinafsi. Tukizingatia kuwa hakuna hakikisho thabithi katika maisha ni wajibu wa kila mmoja wetu kufanya yote tuwezayo ili kuimarisha kinga zetu. Kwa njia hiyo tutakua tumejiandaa vilivyo kuzuia virusi na viini vinavyosababisha magonjwa.

Piracy-free
Assured Quality
Secure Transactions
Delivery Options
Please enter pincode to check delivery time.
*COD & Shipping Charges may apply on certain items.