<p>Vitimbi vya Mama wa Kambo Wivu Radhi za Wazazi Ra?ki Maluuni Mchumba Kaka na Adui Mama ni hadithi zinazosawiri jamii alimochipukia mwandishi au kuishi na kufanya kazi akiwa polisi mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio katika nchi za Tanzania Rwanda Burundi na Uingereza kwa takriban miaka 40. Kitabu hiki ni matokeo ya maombi ya watu wengi waliomsikiliza akizisimulia katika kipindi cha Hadithi na Muziki cha Redio Rwanda katika miaka ya 1980 na 1990. Hadithi hizi pia zimekuwa zikitumiwa na wakuza mitaala wa Kiswahili nchini Rwanda shuleni na zimewafurahisha wapenzi wengine wa fasihi nje ya shule.</p>